Baraza la Waislamu humu nchini (Supkem) limesema kwamba ripoti ya Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo ilifeli kuafiki matarajio ya Wakenya, hasa katika kuangazia namna za kuimarisha gharama ya maisha nchini.

Mwenyekiti wa baraza hilo Hassan Ole Naado katika kikao na waandishi wa habari siku ya Jumapili, alieleza kwamba hata ingawa baadhi ya mapendekezo yanakubalika, suala la gharama ya maisha lilifaa kupewa kipaumbele katika mazungumzo hayo, na kuhakikisha kwamba wananchi wanapunguziwa mzigo mkuwa wa ushuru ulio katika sheria ya fedha ya mwaka wa 2023.

Supkem aidha imetaka serikali kupunguza ushuru unaotozwa katika bidhaa za msingi, ili kuwawezesha wakenya kumudu matumizi ya siku kwa siku, huku pia ikitaka ushuru wa ujenzi wa nyumba kutupiliwa mbali.

December 4, 2023