By Isaya Burugu,Oct 10,2022- Rais  William Ruto hivi leo amekutana na kufanya mazungumzo kana rais wa Tanzania Samia Suluhu katika ikulu ya Dare salaam.

Kwenye mkutano huo uliyohudhuriwa pia na mawaziri mbali mbali kutoka mataifa haya mawili,Rais  Ruto na Samia wamekubaliana kuhusu maswala mbali mbali yanayohitajika kufanywa ili kuzifaa nchi hizi mbili.

Swala la kwanza limekuwa kumaliza ujenzi wa mbomba la kusafirisha gesi kutoka Eneo la Mtwara Tanzania hadi Mombasa nchini Kenya baada ya Ujenzi wa muradi huo kuzinduliwa kati ya rais Samia na rais aliyestaafa wa keyna Uhuru Kenyatta .Swala la kuondoa vikwazo vya mipkani kati ya Kenya  na Tanzania pia litapewa kipau mbele huku rais Wiliamu Ruto akisifia hatua zilizopigwa kufikia sasa katika kutatua swala hilo.

Viongozi hao aidha wamekubaliana kuandaa mkutano wa mawaziri husika kutoka nchi zote mbili kabla ya mwisho wa mwaka ili kutathmini jinsi ya kuharakisha baadhi ya maswala yanayonuiwa kutekelezwa kwa pmaoja.Rais Ruto yuko nchni Tanzania kwa ziara ya siku mbili kufuatia mwaliko na mwenyeji wake rais Suluhu Samia.

October 10, 2022