By Isaya Burugu/BBC ,Oct 10,2022Milipuko kadhaa imesikika katika mji mkuu wa Ukraine Kyiv.Haya ni kwa mjibu wa Ripoti za vyombo vya Habari.Mashambulizi hayo yanajiri siku mbili baada ya daraja pekee linalounganisha Urusi na Crimea inayokaliwa kimabavu na nchi hiyo kushambuliwa.

Hapo jana, Rais Vladimir Putin alilaumu idara za ujasusi za Ukraine kwa kile alichokiita kitendo cha kigaidi.Anatarajiwa kuongoza kikao cha baraza lake la usalama leo kujadili mlipuko huo.Maafisa wa Ukraine wanasema idadi kubwa ya watu wamejeruhiwa katika mashambulizi ya makombora huko Zaporizhzhia usiku kucha.

Mashambulizi ya makombora yanayoendelea katika mji huo kusini mwa Ukraine yamesababisha vifo vya makumi ya raia katika siku za hivi karibuni, huku kukiwa na msukumo unaoendelea kutoka kwa Ukraine kutwaa tena ardhi ya kusini na mashariki inayodhibitiwa na Urusi.

 

October 10, 2022