BY ISAYA BURUGU,21ST NOV,2023-Rais Wiliam Ruto hivi leo amelihutubia bunge la umoja wa ulaya jijini Strathburg nchini Ufaranza.

Rais Ruto amesisitiza kujitolea kwa Kenya,katika kufanya kazi na mataiafa ya bara ulaya ili kuboresha uhusiano wakibiashara zilizo muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya mungano wa ulaya na bara la Afrika.

Aidha rais ameliambia bunge hilo kuwa Kenya inalitegemea katika kukabili visa vya ugaidi vinavyotekelezwa na makundi kama vile Alshabaab na misuko suko nchini Sudan na Somalia.

Rais pia ameguzia hali tete nchini Haiti na kusisitiza haja ya juhudi zote kuelekezwa huko kufanikisha mikakati ya kurejesha utulivu.

 

 

 

 

 

Share the love
November 21, 2023