BY ISAYA BURUGU 23RD DEC 2022-Aliyekuwa  waziri wa uchukuzi  Michael Kamau amerejea tena katika utumishi wa umma  baada yake kuteuliwa mwenyekiti mpya wa bido ya hazina yakitifa yakimatibabu NHIF.
 

Kupitia  notisi  kwenye gazeti rasmi la serikali  iliyochapishwa na rais William Ruto  hivi  leo  jukumu la Kamau  jipya linaanza  leo na litakamilika katika muda  wa miaka mitatu.

 

 Kamau  anachukua mahala pa  Lewis Nguyai aliyehudumu  kwenye wadhifa huo  tangu feburuari  mwaka jana  baada  yake kuteuliwa na aliyekuwa rais  Uhuru Kenyatta.

Lewis Nguyai  alikuwa  mbunge  wa eneo  bunge la Kikuyu.

Rais  Ruto pia amemtuea  aliyekuwa mkuu wa majeshi  Julius Karangi  kama  mwenyekiti  wa  bodi ya baraza  la kitaifa  la  idadi  na maendeleo .

Aidha  Karangi anachukua nafasi  ya aliyekuwa wa Kinangop    David Ngugi aliyechaguliwa  mwezi mei  2021. Karangi atahudumu  hadi  tarehe 20  mwezi Julai.

Kwingineko  rais  Ruto amemteua   aliyekuwa mgombea wa ugavana wa  Nyamira   Walter Nyambati  kama  mwenyekiti  wa bodi  ya Geothermal Development Company, kwa muda wa miaka mitatu.

December 23, 2022