BY ISAYA BURUGU 22ND DEC 2022-Rais  William Ruto amemteua aliyekuwa jaji mkuu  David Maraga kama mwenyekiti wa jopokazi litakalotathmini jinsi ya kuimarisha mazingira ya utendakazi kwa  polisi na maafisa wa magereza.Maraga atasaidiwa  na Carole Karuiki  kwenye jopokazi hilo lililo na wananchama 20.

Aliyekuwa katibu mkuu msimamizi  Moffat Kangi, John Ole Moyaki, Ibrahim Jillo Guyo, Richard Kirundi, Elizabeth Mueni na  Roseline Odede watakuwa sehemu ya jopokazi hilo.Wengine ni ; Joash Odhiambo Dache, Doreen Muthaura, Albert Mwenda, Terry Chebet Maina, Hassan Sheikh Mohamed, Capt. (Rtd.) Simiyu Werunga, Mutuma Ruteere , Anne Ireri, Stephen Kayongo, Jafaar Mohamed, Sammy Chepkwony na  Khadija Mire.

Omwanza Ombati, Joy Mdivo Masinde, Rosemary Kamau watahudumu kama  makatibu wa jopokazi hilo kwa pamoja.

 

Jopokazi hilo linatarajiwa  kuchunguza na kutambua changamoto za kisera,kisheria,usimamizi   kati ya nyingine  zinazotatiza utoaji huduma bora kwa polisi  na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kuzitatua changamoto hizo.

Aidha jopokazi hilo  linahitajika  kutathimini na kutoa mapendekezo kuhusu kuimarisha mazingira ya utenda kazi kwa polisi katika vitengo vyote  sawa  na maswala yote yanayosababisha idara ya polisi kutotekeleza majukumu yake ipasavyo.

 

 

December 23, 2022