Radio Osotua › Local News

Rais Wiliam Ruto atangaza kuwa wakongwe kupata mgao wa fedha zao kabla ya watumishi wa umma kuanzia Juni Mosi

Local News April 4, 2023 Osotua

BY ISAYA BURUGU  4TH APRIL,2023-Rais Wiliam Ruto ruto ametangaza kuwa kuanzia tarehe moja mwezi Juni mwaka huu mgao wa fedha zilizotengwa wazee na makundi mengine hitajika katika jamii zitaanza kutolewa kabla ya mishahara ya watumishi wa umma.Akizungumza katika kongamano la kulinda maslahi ya jamii jijini Nairobi,rais amesema wakati umefika kwa taiafa hili kutekeleza maswala yote na vigezo vilivyopitishwa kisheria kwa minajili ya kijamii

.Rais amesema tayari serikali imetenga shilingi bilioni 28 zitakazowasaidia watu walio na ulemavu ,wazee na  watu wengine wenye mahitaji maalum.

Akiwa shukuru  wafadhili mbali mbali ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kusaidia kenya kuafikia malengo yake,rais ameagiza mabunge yote nchini kuhakikisha kuwa yanashughulikia sera na  sheria zote hitajika kuhakikisha kuwa haki za watu wenye mahitaji maalum wakiwemo wakongwe zinatekelezwa. .