BY ISAYA BURUGU,21ST OCT,2023-Rais wa Angola Joao Lurenco amepokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Wiliam Ruto anapoanza ziara rasmi ya siku mbili humu nchini.Hafla ya kumpokea rais huyo imeandaliwa katika ikulu ya Nairobi asubuhi ya leo na kuongozwa na rais Ruto.

Gwaride la heshima pia limeandaliwa na vikosi mbali mbali vya majeshi ya Kenya kwa niaba ya  rais Laurenco huku miziga 21 ikifyatuliwa.

Akiwa humu nchini rais huyo wa taiafa la Afrika magharii atandaa mazungumzo na rais Ruto kuhusu maswala mbali mbali ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili kwenye Nyanja za kibiashara,kiuchumi ,uwekezaji na vikwzo vya usafiri katia ya raia wa mataiafa hayo mawaili ili kurahizisha uhusiano.

 Wakati huo huo Rais Wiliam Ruto na mwenzake wa Angola Joao Lourenco wameafanya mazunguzo katika ikulu ya Nairobi hivi leo huku rais wa Angola akianza ziara rasmi ya siku mbili humu nchini.Katika mazunguzmo hayo viongozi hao wameafikia kufufua tena safari za ndege za moja kwa moja kutoka HUMU NCHINI hadi nchini Angola kama njia moja ya kuboresha utendaji biashara na uhusiano baina ya raia wa mataiafa hayo.

Aidha rais Ruto amemhakikishia rais Lourenco kuwa Kenya itaendelea kutekeleza jukumu lake katika kuleta amani na utulivu nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Share the love
October 21, 2023