BY ISAYA BURUGU,21ST OCT 2023-Maafisa wa polisi katika kaunti ya Tharaka Nithi wameanzisha uchunguzi kufutia vifo vya wanafunzi wawili wa shule ya upili baada yao kudaiwa kunywa pombe iliyo kuwa na kemikali aina ya Ethanol.

OCPD wa eneo la Muthambi John  Ole Manei amedhibitisha kisa hicho.

Afisa huyo   vilevile amesema kuwa wanafunzi hao ni wa shule ya Karigini iliyoko wadi ya Muthambi eneo bunge la Muthambi kaunti ya Tharaka Nithi.

Wanafunzi hao wanaripotiwa kupelekwa hospitalini wakiwa hali mahututi na kuaga dunia walipokuwa wakihudumiwa na madakitari.

 

 

 

 

 

 

 

Share the love
October 21, 2023