Rais William Ruto amefungua rasmi kongamano la ugatuzi la mwaka 2025 katika kaunti ya Homabay. Katika hotuba yake, rais Ruto ametambua serikali za kaunti kama chombo muhimu katika kuchangia maendeleo ya kitaifa na mashinani.

    Vilevile amesema kuwa kauli mbiu ya kongamano hilo ujumuishaji na usawa, unawiana na ruwaza ya kitaifa ya kuhakikisha usawa katika masuala yote.

    Aidha mkuu wa nchi amesema kuwa mabadiliko ya kitaifa yanatatizwa na ufisadi, akisisitiza kwamba ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa fedha za umma zinatumika ipasavyo kwa manufaa ya wakenya wote.

    August 13, 2025

    Leave a Comment