Rais William Ruto hii leo amezindua na kufungua miradi mbalimbali katika maeneobunge ya Narok mashariki na Narok kaskazini ikiwemo soko la kisasa huko Suswa na ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa kataifa katika eneo la Iloisiusiu.
Rais Ruto kando na kuzindua miradi hiyo, ameikabidhi serikali ya Narok hatimiliki ya ardhi ya Mau, hatua ambayo anadai itamaliza mzozo ambao umekuwa ukizunguka ardhi hiyo kwa muda mrefu.
Kando na hayo, rais Ruto amesema kuwa Serikali itaendelea kuuzingira Msitu wa Mau ili kuzuia uvamizi na shughuli zingine haramu. Kulingana na mkuu wa nchi, hatua hiyo itasaidia kulinda mipaka ya msitu huo.
Zaidi ya hayo, alipokuwa akiwahutubia wakazi wa Suswa, Rais alitaja kuwa utawala wake pia unashughulikia suala la shamba la Ewaso Kedong kwa kuwagawia wenyeji ardhi zaidi.
Viongozi walioandamana na rais William Ruto wakiongozwa na gavana wa Narok Patrick Ntutu wameelezea furha yao kufuatia hatua hiyo wakisema kuwa kwa muda mrefu msitu huo umekuwa ukipoteza hadhi yake kutokana na shuguli za kibinadamu.
Groundbreaking Ceremony for Narok International Airport. https://t.co/tyiW28B2wl
— State House Kenya (@StateHouseKenya) May 6, 2025