Mawaziri, Makatibu Wakuu, na Baraza la Washauri wamekusanyika katika Kituo cha Mikutano cha Edge huko South C jijini Nairobi, kwa mkutano wa siku mbili.

Mkutano huo unatumika kutafakari mwaka wa kwanza wa Kenya Kwanza madarakani huku kukiwa na wasiwasi kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha na ushuru wa kupindukia.

Akifungua mkutano huo rasmi, Rais William Ruto amesema atafanya maamuzi sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi akidai kuwa mwelekeo wa serikali ni wa muda mrefu na kwa manufaa makubwa zaidi ya wananchi. Rais alibainisha kuwa hatafuata njia ya mkato inayopendwa na watu wengi bali ya kukosoa na yenye kuleta mabadiliko.

November 16, 2023