Ufichuzi wa gazeti la daily Nation kuhusu ujenzi wa kanisa ndani ya ikulu ya rais jijini Nairobi, mradi unaokadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi 1.2B umeibua hisia mseto miongoni mwa baadhi ya wakaazi wa mji wa Narok.

    Kwa mujibu wa wakaazi hao ambao wamezungumza na wanahabari wetu, fedha hizo zinaweza kutatua changamoto zinazokumba taifa la Kenya mojawapo ikiwa ukosefu wa dawa hospitalini.

    Vilevile wanahisi kuwa kutumia kiasi kikubwa cha fedha kujenga kanisa kwa sasa ni kutojali matatizo ya msingi ya mwananchi wa kawaida.

    Aidha wamesisitiza kuwa hawapingi dini wala maombi, bali wanapinga miradi ambayo haijakadiriwa kwenye bajeti ya taifa.

    Hata hivyo kuna wale ambao wanaunga mkono hatua hiyo wakisema kujengwa kwa kanisa ndani ya ikulu ni hatua ya kipekee ya kudumisha maombi katika uongozi wa taifa.

    Hata hivyo rais William Ruto amejibu ufichuzi huo akieleza kwamba hajutii kabisa kulijenga kanisa hilo.

    Katika matamshi yake ambayo yameonekana kuwasuta watu wanaomkosoa, rais Ruto amesema kuwa fedha za serikali hazijatumika katika ujenzi wa kanisa hilo huku akishikilia kuwa hataomba msamaha kwa yeyote.

    July 4, 2025

    Leave a Comment