Rais William Ruto amesisitiza kuwa hakutakuwa na kesi za ufisadi katika serikali yake huku akipanga kutekeleza ahadi alizotoa kwa Wakenya.

Akizungumza wakati wa shuguli ya mawaziri kutia saini kandarasi za utendakazi katika Ikulu hii leo, Rais Ruto alisema kuwa viongozi kwa muda mrefu wametumia vibaya umaarufu wao na afisi zao kupora pesa za umma.

Aliongeza, kwamba hali hiyo imeondoa imani ya Wakenya kwa utendakazi wa serikali. Kwa upande wake naibu Rais Rigathi Gachagua aliwakashifu Mawaziri kwa kutozungumzia hatua ambazo wizara mbalimbali zimepiga tangu rais William Ruto alipochukua atamu za uongozi.

Akizungumza katika Ikulu, Gachagua alisema kuwa Mawaziri wengi hawaonyeshi mafanikio ya serikali. Aliendelea kudokeza kuwa vyombo vya habari vimekuwa vikijaribu kuwafikia baadhi ya Mawaziri lakini wanaishia kutojitokeza kwa mahojiano.

Wiki iliyopita,bunge la Seneti lilighadhabishwa baada ya mawaziri watatu kukosa kufika mbele ya maseneta. Watatu hao ni wakiwemo Florence Bore (Leba), Alfred Mutua (Masuala ya Kigeni) na Susan Nakhumicha (Afya)

 

Share the love
August 1, 2023