Rais William Ruto hatimaye amevunja kimya kuhusu sakata ya ufadhili wa masomo ya Finland na Kanada katika kaunti ya Uasin Gishu.

Rais Ruto ameahidi kuwa serikali itawasaidia wanafunzi ambao walilaghaiwa na mpango huo wa ufadhili wa masomo.

Kulingana na Ruto, serikali itawachukuliwa hatua za kisheria wote waliohusika kwenye sakata hiyo.

wakati huohuo seneta Jackson Mandago aliyekuwa gavana Uasin Gishu wakati wa tukio hilo alitiwa mbaroni saa chache baada ya agizo la kukamatwa kwake kutolewa na mahakamani.

Alikamatwa katika makazi yake na kusafirishwa hadi afisi ya DCI mjini Nakuru. Seneta huyo ni miongoni mwa watu wengine watatu wanaokisiwa kuhusika katika Mpango wa Elimu wa Finland na Kanada, ambao umekumbwa na utata.

Viongozi wengine ni Joseph Kipkemoi Maritim, Meshak Rono na Joshua Kipkemoi Lelei. Mahakama ya Nakuru ilitoa agizo hilo la kukamatwa hii leo ili aweze kujibu mashtaka mbalimbali.

Mandago, pamoja na washtakiwa wenzake, wameshtakiwa kufuja Ksh.1.1 bilioni kutoka kwa akaunti ya Benki iliyosajiliwa chini ya Uasin Gishu Education trust Fund na iliyokusudiwa kulipia karo ya wanafunzi waliosajiliwa kwenye mpango huo.

Hivi majuzi mamia ya wanafunzi pamoja na wazazi wao waliandamana wakidai kurejeshewa fedha walizolipa kwa ajili ya mpango huo.

Share the love
August 16, 2023