BY ISAYA BURUGU 17TH AUG 2023-Seneta wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago Uasin na watuhumiwa  wengine  wawili wameachiliwa huru kwa dhamana ya shilingi nusu milioni au bondi ya shilingi milioni mbili.

Wakifika mbele ya mahakama kuu ya Nkuru leo ,hakimu mkuu wa mahakama hiyo Alloyce Ndege ametoa uamuzi kuwa watatu hao warejee mahakamani baadaye ili kujibu au kukanusha.Seneta huyo ni miongoni mwa watu wengine tatu Joshua Lelei  Mishack Rono, na  Joseph Maritim.

Watatu hao wanatuhumiwa kupanga njama ya kuiba shilingi bilioni 1.1  kutoka kwa akaunti ya benki ya Kenya commercial mjini Eldoret  iliyosajiliwa chini ya hazina ya ufadhili wa elimu ya kaunti ya Uasin Gishu Education Trust Fund,iliyokusudiwa kuwalipia wanafunzi karo kusomea vyuo vikuu vya Finland na Canada.Mutuhumiwa wa tatu Joseph maritim hakuwepo mahakamani baada ya taarifa kuibuka kuwa yuko nje ya nchi.Wakili wake Sam Yego ameiomba mahakama kumwachilia mteja wake kwa masharti sawia na kuondoa kibali cha kutaka akamatwe.

.Huku mamia ya wanafunzi na wazazi wao walioadhirika wakimiminika katika Barabara za mji wa Eldoret kuitisha kurejeshewa fedha zao kutoka kwa serikali ya kaunti,skata hiyo imezua malumbano makali katika kaunti ya uasin Gishu.

August 17, 2023