BY ISAYA BURUGU,17TH AUG 2023-Seneta wa kaunti ya Uasin Gishu Jackson Mandago amefikishwa mahakamani asubuhi ya leo  kuhusiana na Sakata ya mpango wa ulipaji karo kwa elimu ya wanafuzni maskini katika kaunti ya Uasin Gishu  Sakata ambayo imekumba kaunti hiyo kwa majuma ya hivi karibuni.

Seneta  Mandago  amefikishwa katika mahakama kuu ya Nakuru  Pamoja na watuhumiwa wengine wawili  Joshua Lelei na  Mishack Rono, kwasababu mtuhumiwa wa tatu Joseph Maritim, kwa sasa yuko nje ya nchi.

Watatu hao wanatuhumiwa kupanga njama ya kuiba shilingi bilioni 1.1  kutoka kwa akaunti ya benki ya Kenya commercial mjini Eldoret  iliyosajiliwa chini ya hazina ya ufadhili wa elimu ya kaunti ya Uasin Gishu Education Trust Fund,iliyokusudiwa kuwalipia wanafunzi karo kusomea vyuo vikuu vya Finland na Canada.

Akifika mbele ya idara ya upelelezi wa jinai DCI jana ,seneta huyo alihojiwa kabla ya kuhamishiwa katika kituo cha polisi cha central jijini Nakuru  ambapo amekesha usiku kucha.

Huku mamia ya wanafunzi na wazazi wao walioadhirika wakimiminika katika Barabara za mji wa Eldoret kuitisha kurejeshewa fedha zao kutoka kwa serikali ya kaunti,skata hiyo imezua malumbano makali katika kaunti ya uasin Gishu.

 

 

 

 

August 17, 2023