Rais William Ruto ametangaza mfumo mpya wa serikali wa kuwafidia raia na maafisa wa usalama waliopata majeraha au kupoteza maisha wakati wa maandamano ya umma nchini tangu 2017.
Katika tangazo la rais lililotolewa Ijumaa, Ruto alisema mpango huo unalenga kusawazisha uhuru wa kikatiba na uwajibikaji wa kiraia, huku akishughulikia gharama za kibinadamu na kiuchumi za machafuko ya kisiasa.
Taarifa hiyo ilibainisha kuwa mpango huo wa siku 120 utaratibiwa na Ofisi ya Rais kwa ushirikiano na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Wizara ya usalama wa Ndani, wizara ya Hazina ya kitaifa na vyombo vingine muhimu vinavyohusika.
Rais Ruto alimtaja Prof. Makau Mutua, Mshauri Mkuu wa Masuala ya Kikatiba na Haki za Kibinadamu, kuwa mratibu mkuu wa zoezi hilo maalum la ulipaji fidia.
Fidia ya waathiriwa wa maandamano pamoja na kuhifadhi haki ya kuandamana kwa amani ilikuwa miongoni mwa ajenda 10 zilizokubaliwa na Rais Ruto na Raila Odinga katika kuunda serikali pana.
— William Samoei Ruto, PhD (@WilliamsRuto) August 8, 2025