BY ISAYA BURUGU 20TH JULY 2023-Shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini la Haki Africa limewataka viongozi walioko serikalini na wale wa upinzani kuketi katika meza ya mazungumzo ili kufikisha kikomo mandamano yanayo shuhudiwa nchini.

Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo  Hussein Khalid amelezea kusikitishwa kwake na hasara iliyopatikana kufuatia mandamano hayo ikiwemo kupotea kwa Maisha.Pia amewakosoa polisi vikali kwa kutumia nguvu kupita kiasi.

Afisa huyo pia anaitaka serikali na taasisi zake kuheshimu mahakama na kusitisha kikamilifu utekelezaji wa sheria ya kifedha yam waka 2023.

.

 

 

 

Share the love
July 20, 2023