BY ISAYA BURUGU ,16TH NOV 2022-Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula, ametangaza kusitishwa kwa zoezi la kuwapiga msasa Makatibu Wakuu walioteuliwa, kufuatia agizo la mahakama ya leba kusitisha zoezi hili, ili kupisha kusikilizwa na kuamuliwa kwa kesi iliyowasilishwa na chama cha wanasheria nchini LSK.

Kulingana na taarifa iliyotolewa mapema leo na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula, Bunge hilo lina wajibu wa kujitika katika sheria na kuzingaia utawala wa sheria na kwa hivyo kueleza kuwa bunge limeridhia kuahirisha mchakato huo wa uhakiki hadi kesi hiyo itakapoamuliwa.

Katika agizo la mahakama, Kamati za Idara mbalimbali za bunge, ambazo zilianza mchakato wa kuwapiga msasa makatibu wateule siku ya Jumatatu, pia zimepigwa marufuku dhidi ya kutoa taarifa ya zoezi hilo kwa Bunge.

 

November 16, 2022