Rais William Ruto amejitenga na semi za kubadilisha katiba zilizotawala vyombo vya habari majuma mawili yaliyopita.

Akizungumza baada ya kikao na wajumbe wa chama cha UDA katika ikulu ya Nairobi, Ruto amesema kwamba hatajihusisha kwa vyovyote na shughuli zilizo na nia ya kuhitilafiana na katiba au kuifanyia mabadiliko kwa manufaa ya kisiasa. Kauli yake inajiri baada ya kauli ya mbunge wa Fafi Salah Yakub, aliyependekeza kubadilishwa kwa katiba ili kuruhusu rais kuongoza kwa zaidi ya mihula miwili iliyotolewa sasa na katiba ya taifa.

Ruto ameongeza kuwa wabunge wana haki yao ya kutoa maoni ila akaahidi kujitenga na semi zozote za aina hiyo.

November 16, 2022