Baraza la magavana limetoa taarifa kinzani kuhusu tangazo la wizara ya afya kwamba wahudumu wa afya chini ya mpango wa afya kwa wote UHC wataajiriwa kuanzia septemba mwaka huu.

    Kupitia taarifa kwa vyombo vya habari, mwenyekiti wa kamati ya afya katika baraza la magavana Muthomi Njuki, ameeleza kuwa baadhi ya masuala yaliyotangazwa na wizara ya afya hayakujadiliwa wakati wa mkutano kati ya ngazi hizo mbili.

    Vilevile ameongeza kuwa mchakato wa kuwaajiri wahudumu hao kwa mikataba ya kudumu na pensheni, haukuwa umeafikiwa rasmi. Njuki ameshikilia kwamba mchakato huo utaendelea iwapo tu fedha zilizoahidiwa zitatolewa ili kufanikisha uajiri wa wahudumu hao Zaidi ya 7,000.

    August 26, 2025