BY ISAYA BURUGU,24TH OCT 2023-Hali ya taharuki imetanda katika eneo la
Kapindasum  baada ya washukiwa wa ujambazi kuzingira kambi ya maafisa wa polis  Baringo ya kusini
.

Taarifa pia zinaarifu kuwa majangili hao wamezingira shule ya msingi ya  Kapindasum na kusababisha hofu .Kwa mjibu wa Chifu wa lokesheni ya Arabal Wiliam Koech makabiliano ya risasi katoi ya majangili hao na maafisa wa polisi wa GSU yanaendelea.

Kisa hiki kinajiri wiki tatu baada ya majangili kuvamia shule ya msingi ya Kapindasum na kuanza kufyatua risasi wakati wanafunzi walipokuwa wakwenda kusaka chakula cha mchana.

 

 

October 24, 2023