TSC

BY ISAYA BURUGU,13TH OCT 2023-Walimu wasio wenyeji na ambao wamekuwa wakitafuta uhamisho kutoka Kaskazini Mashariki mwa Kenya kutokana na ukosefu wa usalama wamepata pigo kubwa baada ya Tume ya Kuajiri Walimu kuwaachisha kazi kwa kutoroka kazini.

Hii inafuatia agizo la tume mwezi Septemba kwa walimu hao kurejea katika vituo vyao vya kazi.Walimu hao wanashutumu TSC kwa kukiuka mamlaka yake na sasa wanasema watapiga kambi nje ya makao makuu ya tume hiyo wiki ijayo huku wakiomba bunge kuingilia kati.

Katika barua zilizotumwa kwa walimu walioathiriwa TSC ilitaja hatua hiyo ya walimu kukataa kuripoti kazini kama ukiukaji wa Sheria za Tume ya kuajiri walimu (TSC).

Kwa wiki kadhaa, walimu hao wamekuwa wakipiga kambi katika Makao Makuu ya TSC wakitaka kuhamishwa kutoka eneo hilo, wakitaja ukosefu wa usalama kutokana na tishio la ugaidi la Al-Shabaab na uhasama kutoka kwa jamii ya eneo hilo. Walimu hao wanasema TSC haijali masuala wanayoibua.

 

 

Share the love
October 13, 2023