Mhubiri wa kanisa la New life centre Ezekiel Odero hii leo alifika mbele ya kamati ya seneti inayochunguza mauaji ya shakahola ili kujibu maswali kuhusu kanisa lake ambalo lilikisiwa kuwa na uhusiano na kanisa la Mhubiri Paul Mckenzie.

Odero akizungumza mbele ya kamati hiyo, amewaalika maseneta hao kutembelea kanisa lake ili kufanya uchunguzi na kuandika ripoti kulingana na kile watakachoona.

Kuhusiana na suala la mhubiri Mckenzie, Odero amefichua kuwa walikutana mara moja wakati ambapo alinunua kituo cha runinga kutoka kwake ila akakanusha madai kuwa wamewahi kushiriki kwenye madhabahu sawa na Mckenzie.

October 13, 2023