BY ISAYA BURUGU,08 NOV,2022-Warsha ya kupambana na ufisadi katika vyama vya ushirika na mashirika mengine ya kijamii imeingia siku ya pili leo huko Mombasa.

Warsha hiyo inalenga kuziba mianya ya ufisadi haswa ikizingatiwa kuwa serikali inalenga kutumia vyama hivyo kusambaza fedha kutoka kwa hazina ya husler.

Warsha hiyo imewaleta Pamoja maafisa wa tume ya kupammbana na ufisadi nchini EACC na wale wanaotoka kwenye vyama tofauti vya ushirika kuwapa mawaidha kuhusu kukabili ufisadi .Huyu hapa Mark Ndiema ambaye ni afisa mshirikishi wa tume ya EACC ukanda wa pwani

.Rais Wiliam Ruto anatarajiwa kuzindua rasmi hazina hiyo ya husler tarehe mosi mwezi ujao.Joseph Osoro ni afisa kutoka halmashauri ya kudhibiti vyama vya ushirika nchini.

November 8, 2022