BY ISAYA BURUGU,08 NOV,2022Japheth Koome aliyetuliwa kama inspekta mkuu wa polisi amesema kuwa nia yake ni kuhakikisha kuwa idara ya polisi inafanya kazi ipasavyo huku akilenga kutetea maslahi ya maafisa wa polisi.Akizungumza alipofika mbele ya kamati ya uteuzi bungeni kupigwa msasa Koome amelezea Imani kuwa ujuzi aliyoupata akihudumu katika nyadhifa zingine husika utampa uwezo Zaidi kutekeleza jukumu lake.

Koome amekuwa mkurugenzi mkuu wa taasisi ya mafunzo kwa polisi huko Kiganjo.Pia hapo nyuma aliwa kuwa kamanda wa polisi wa Nairobi. Kuhusu kiini cha fedha zake ni uwekezaji  wa hisa katika vyama kadhaa vya ushirika ikiwemo chama cha ushirika cha polisi.

Pia anamiliki trekta mbili na yeye ni mkulima.Katika kaunti ya Meru anakotoka,Koome ameiambia kamati ya bunge kuwa ana Ekari saba za ardhi vipande viwili vya ardhi kule ambakasi na kipande cha ardhi Nairobi anakoishi.

 

 

November 8, 2022