Uchunguzi wa kifo cha Albert Ojwang, umeanzishwa ili kubaini kiini cha kifo chake na matukio yaliyochangia kuaga kwake chini ya ulinzi wa polisi.

    Inspekta jenerali wa polisi Douglas Kanja, akiwahutubuia waandishi wa habari mapema leo, katika kituo cha polisi cha Central ambako Ojwang’ alizuiliwa, alisema kuwa maafisa wa polisi waliokuwa kwenye zamu wakati wa tukio hilo wamesimamishwa kazi ili kutoa nafasi ya uchunguzi bila hitilafu yoyote.

    Aidha, Kanja alishikilia dhamira ya huduma ya kitaifa ya polisi NPS katika kuhakikisha sheria inafuatwa na haki za binadamu zinalindwa.

    Kwa upande wake mwenyekiti wa mamlaka ya kutathmini utendakazi wa polisi IPOA Isack Hassan, alikiri kupokea taarifa kuhusu kisa hicho, huku akitoa hakikisho kwamba mamlaka hiyo itafanya kila iwezalo kuona kuwa haki imetendeka.

    June 9, 2025

    Leave a Comment