BY ISAYA BURUGU 15TH FEB 2023-Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ameteuliwa kuongoza ujumbe wa wanachama 90  kutoka mungano wa Afrika wataokuwa wangalizi wa uchaguzi mkuu nchini Nigeria.

Uchaguzi huo unaratibiwa  kufanyika tarehe 25 mwezi huu.Kupitia taarifa Au imesema Kenyatta ataongoza ujumbe huo wa muda mfupi unaojumuisha nchi mbali mbali wanachama ,mashirika ya haki za kijamii kati ya mengine.

Jukumu la ujumbe huo ni kutoa taarifa za hakika na sisizoegemea upande wowote kwenye uchaguzi huo kwa kuzingatia vigezo kama vile uwazi wa zoezi lenyewe nak ama uchaguzi huo umetimiza viwango hitajika kidemokrasia kuambatana na vigezo vya nchi wannachama.

Nigeria inaelekea katika uchaguzi katika muda wa siku kumi zijazo,wakati ambapo imekumbwa na changamoto mbali mbali zikiwemo ukosefu wa usalama,fedha na hata mafuta.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

February 15, 2023