Viongozi mbalimbali wa kidini nchini walikusanyika katika uwanja wa Nyayo kuanzia asubuhi ya leo, kwa hafla ya maombi yaliyoandaliwa kwa nia ya kuliombea taifa.

Viongozi wa serikali wakiongozwa na Rais William Ruto na Naibu wake Rigathi Gachagua walihudhuria hafla hii ambayo dhima kuu ilikuwa ni kuomba mvua katika taifa la Kenya. Katika hotuba yake wakati wa hafla hii, Rais Ruto alieeleza kuwa viongozi wa Kidini wamepata kufahamu mwelekeo wanaofaa akuchukua kwa kuliombea taifa, akiweka bayana kwamba maombi ya wakenya yatasikika ili Wakenya waweze kuepuka makali ya kiangazi kinachowalemea wakenya wengi kutoka pembe tofauti za dunia.

Aidha Rais Ruto alieleza mipango kabambe ya kubadilisha maisha ya mkenya wa kawaida, akisema kwamba ameyawasilisha yote haya mbele ya Mungu akiendelea kuyatekeleza ili kuwakwamua wakenya.

February 14, 2023