Hussein Mohammed

    Rais William Ruto amefanya uteuzi wa maafisa 10 wapya katika Afisi Kuu ya Rais Ijumaa 14.10.2022. Katika orodha ya uteuzi huo, Rais amemteua aliyekuwa mwanahabari wa Runinga ya Citizen Hussein Mohammed kama msemaji wa Ikulu huku mwanauchumi David Ndii akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la washauri wa Rais kuhusu maswala ya Kiuchumi. Orodha kamili ya watu walioteuliwa inajumuisha

    Felix K. Koskei – Mkuu wa Wafanyakazi na Mkuu wa Utumishi wa Umma

    Aliyekuwa gavana wa Turkana Josphat Nanok – Naibu Mkuu wa Wafanyakazi

    Dkt. Augustine Cheruiyot – Mshauri Mkuu & Mkuu wa Sekretarieti ya Mabadiliko ya Kiuchumi

    Dkt. Kamau Thugge – Mshauri Mkuu na Mkuu wa Masuala ya Fedha na Sera ya Bajeti

    Mohammed Hassan na Nancy Laibuni – Mjumbe, na Mjumbe mshirikishi wa Baraza la washauri wa rais katika maswala ya Kiuchumi

    Katoo Ole Metito – Mdhibiti wa Ikulu

    Bw. David Mugonyi – Mkuu wa Huduma ya Mawasiliano ya Rais

    October 14, 2022