Jumla ya familia 2,500 katika kaunti hii ya Narok zina sababu ya kutabasamu baada ya shirika la msalaba mwekundu kusambaza chakula cha msaada kwa familia hizo.

Kaunti ya Narok ni miongoni mwa kaunti 29 ambazo zimeathirika kutokana na ukame.Katibu mkuu wa shirika hilo la msalaba mwekundu Asha Mohammed ameeleza kuwa Zaidi ya watu milioni 4 nchini wameathirika kutokana na kiangazi.

Naye mkewe naibu rais Dorcus Gachagua ametoa wito kwa wakenya wenye nia njema kutoa misaada ya vyakula kupitia shirika la msalaba mwekundu ili serikali iweze kufikia familia zaidi zilizoathirika.

Aidha hivi majuzi,gavana wa kaunti hii Patrick Ntutu alisema kuwa Zaidi watu laki tatu katika kaunti hii wanakabiliwa na njaa inayotokana na ukame ambao umesababishwa na ukosefu wa mvua.

October 14, 2022