BY ISAYA BURUGU/BBC,10,NOV 2022-Uwanja wa ndege wa Bukoba kaskazini – magharibi mwa Tanzania umefunguliwa tena kufuatia ajali iliyosababisha vifo vya watu 19.

Ndege hiyo ya abiria ilianguka katika Ziwa Viktoria ilipokuwa ikijaribu kutua kwenye uwanja huo Jumapili iliyopita.Afisa utawala katika mji huo amesema  kwamba ndege ya kwanza ya abiria inatarajiwa kutua kwenye uwanja wa Bukoba leo Alhamisi.

Washauri wa kiufundi kutoka kwa watengenezaji wa ndege, ATR, wameanzisha uchunguzi kuhusu ajali hiyo.Wataalamu wa Ufaransa wa usalama wa safari za ndege pia wamepelekwa nchini humo.

Ndege hiyo ilikuwa ni ya kampuni ya Precision Air – kampuni kubwa zaidi ya kibinafsi ya safari za ndege za abiria nchini Tanzania.Imekuwa ikiendesha safari zake kutoka Dare es salaam hadi  Bukoba tangu mwaka 1994

 

November 10, 2022