BY ISAYA BURUGU 10 NOV,20222-Wahudumu wa bodaboda mjini Kisii wamezindua mikakati ya kujihakikishia usalama.Hatua hiyo inafuatia kuongezeka kwa visa vya uhalifu vinavyowahusu wahudumu hao.

Inaripotiwa kuwa wahalifu wamekuwa wakiwaendea wahudumu hao kwenye stendi wakijifanya abiria na wanapobebwa wakifika njiani wanageuka na kuwavamia na kuwaibia wahudumu waliowabeba.

Kufuatia hali hiyo wahudumu hao kupitia viongozi wao wamepanga kutembea stendi moja hadi nyingine kudhibitisha wahudumu wanaoendesha shughuli zao kwenye maeneo .

November 10, 2022