Dorcas Rigathi

Mke wa Naibu Rais Pst. Dorcas Rigathi ameendelea kusisitiza azma yake ya kuwasaidia vijana katika kupambana na changamoto za uraibu wa dawa za kulevya na kusimama kidete katika kutetea maslahi yao, hususan vijana wa kiume nchini.

Haya yalijitokeza baada ya kuhudhuria na kushiriki katika Matembezi ya Kuelimisha Afya ya Akili yaliyofanyika siku ya Ijumaa katika eneo la Gatunyu, Gatanga, Kaunti ya Murang’a. Lengo la matembezi hayo lilikuwa ni kutoa hamasa kuhusu masuala ya afya ya akili pamoja na kujenga ufahamu dhidi ya matumizi mabaya ya vileo na dawa za kulevya katika eneo hilo.

Matembezi hayo yalifuatiwa na sherehe za mahafali kwa vijana waliopokea mafunzo ya kiufundi kupitia ushirikiano kati ya Kanisa Katoliki na jamii. Bi. Dorcas, alitumia hafla hiyo kuishukuru jamii kwa mchango wake katika kupambana na matumizi ya pombe haramu na dawa za kulevya.

YouTube player

Kando na hayo, Pst. Dorcas pia aligusia umuhimu wa afya ya akili kwa jamii na kusisitiza juu ya umuhimu wa kutoa mafunzo ya kuboresha afya ya akili kama njia ya kupunguza visa vya msongo wa mawazo na kujitia kitanzi. Vilevile aliwahimiza vijana kushiriki katika mafunzo haya kwa wingi.

May 25, 2024