Takriban familia 40,000 zinazojumuisha watu 181,000 zimehama kwa hiari kutoka kwa hifadhi za mito ya Nairobi, Mathare na Ngong na vijito vingine vidogo vya mfumo wa Ikolojia wa Mito ya Nairobi.

Haya ni kwa mujibu wa waziri wa usalama wa ndani Kithure Kindiki ambaye amezuru mto Nairobi kukagua shuguli ya uhifadhi wa mto Nairobi.

Kupitia mtandao wake wa X, Kindiki aidha ameeleza kuwa serikali tayari imetimiza ahadi ya Ksh.10,000 kwa kila familia iliyoathirika kutokana na mafuriko katika eneo la Mathare.

Alishikilia kwamba Familia hizo zitapewa kipaumbele katika Mpango wa Nyumba za bei nafuu.

May 24, 2024