Baadhi ya viongozi wa Azimio la Umoja sasa wanaitaka serikali kutimiza ahadi zao walizotoa wakati wa kampeni badala ya kuilaumu serikali iliyopita.

Wabunge hao wakiongozwa na Edwin Sifuna walisema utawala unaoongozwa na rais William Ruto umekuwa ukinyooshea kidole utawala uliopita badala ya kushughulikia masuala yanayowakumba Wakenya wa kawaida kama vile gharama ya juu ya maisha.

Wabunge hao pia walikabiliana na suala la ukopaji wa serikali ya kitaifa, wazo ambalo walilipinga vikali wakati wa kampeni zao.

Aidha wamesema hawatalegea katika azma yao ya kushinikiza serikali iwajibike kuhusu jinsi wanavyotumia pesa za walipa kodi ambazo wanasema zinafujwa. Walikuwa wakihutubia wanahabari katika makao makuu ya chama cha ODM leo mchana.

March 8, 2023