BY ISAYA BURUGU ,25TH SEPT,2023-Viongozi wakisiasa Pamoja na wazee inayojumuisha kaunti za Laikipia,Narok na Samburu na Kajiado hivi leo wameandaa mkutano mjini Nanyuki kaunti ya Laikipia ili kujadili mikakati mwafaka ya kutatua mzozo ambao umeshuhudiwa kwa muda sasa kati  ya  jamii za Samburu na Laikipia.

Wakizungumza na wandishi Habari viongozi hao wanasema wana Imani kuwa mkutano huo utaafikia matunda na kuzileta Pamoja jamii hizo ambazo zimekuwa zikizozana kwa muda mrefu kutokana na uhasama wa wizi wa Mifugo.

Viongozi hao wameongeza kuwa wanafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa jamii hizo zinaishi kwa amani bila kuzozana.

Mbunge wa Samburu mashariki Jackson Lemutare amesema wana Imani mkutano huo utazaa matunza.

 

 

 

 

 

 

Share the love
September 25, 2023