Viongozi wa muungano wa Azimio la Umoja wameeleza nia ya kuchukua hatua Zaidi, kuweka peupe idhibati kwamba rais William Ruto hakuibuka mshindi katika uchaguzi wa mwaka jana.

Wakizungumza katika kikao na waandishi wa habari jioni ya leo, viongozi hao wakiongozwa na kinara wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzake wa Narc Kenya Martha Karua, viongozi hao wamesema kuwa ripoti ya mfichuzi iliyoachiliwa jana imeweka peupe hali duni ya demokrasia humu nchini.

Viongozi hao aidha wameahidi kuchukua hatua Zaidi kinara wa muungano huo Raila Odinga atakaporejea nchini.Wengine waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na katibu wa chama cha Jubilee Jeremiah Kioni, ambaye aliweka wazi taarifa za ufichuzi kuhusu uchaguzi huo wa mwaka jana.

January 19, 2023