Bunge la seneti limeidhinisha mswada wa marekebisho wa tume huru ya uchgauzi na uratibu wa mipaka nchini, ili kupisha kuanza kwa zoezi la kuwateua makamishena wapya wat me hiyo ya IEBC.

Mswada huo umepitishwa bila kufanyiwa mabadiliko yoyote baada ya mwenyekiti wa kamati ya masuala ya kisheria kwenye bunge hilo Hillary Sigei kuondoa mapendekezo ya mabadiliko kwenye mswada huo. Kabla ya vikao vya leo, kulikuwa na pendekezo la kufanya mabadiliko katika jopokazi linalowateua makamishena wa IEBC, uliopendekeza kupunguza baadhi ya nafasi na kutengewa vyama vya kisiasa.

Maseneta 28 walipiga kura kuunga mkono Mswada huo na sasa jopo la uteuzi litakuwa na wanachama 2 wanaoungwa mkono na Tume ya Huduma za Bunge, mwakilishi mmoja kutoka tume ya Utumishi wa Umma, mwakilishi mmoja kutoka kwa chama cha mawakili nchini (LSK) huku baraza la dini mbalimbali likiwa na nafasi ya wanachama wawili.

January 19, 2023