Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen amesema sasa itakuwa ni lazima kwa vituo vya polisi kote nchini kuwa na kamera za CCTV.

    Waziri huyo akitoa taarifa kuhusu hali ya usalama nchini, alifafanua kuwa kamera za CCTV zilizopo katika baadhi ya vituo siyo rasmi na hazijaidhinishwa kikamilifu na Huduma ya Kitaifa ya Polisi.

    Mukomen alisema kuwa OCS wa kituo husika ndiye atakayesimamia udhibiti wa kamera hizo za CCTV. Aliongeza kuwa vituo vyote 1,209 vya polisi nchini vitakuwa na kamera za CCTV ndani ya miaka miwili ili kuboresha uwazi na uwajibikaji katika vitu vya polisi.

    June 16, 2025

    Leave a Comment