Kikao maalum katika bunge la kaunti ya Kericho kilikatizwa baada ya Machafuko kuzuka, baada ya wawakilishiwadi kutofautiana kuhusu uongozi wa nunge hilo.

Katika kanda ya video iliyosambaa mitandaoni, wawakilishiwadi hao wameonekana wakirushiana Makonde huku wengine wakijaribu kuwatenganisha. Viongozi hao walikua wamekongamana katika kikao maalum cha bunge hilo ili kuwatafuta viongozi wa wengi bungeni, baada ya viongozi waliokuwa wamechaguliwa hapo awali kujiuzulu kutoka kwa nyadhifa hizo.

Mnamo Januari 9, mwakilishiwadi wa Kamasian Philip Rono alichaguliwa kuwa kiongozi wa Wengi huku mwenzake wa Kapsuser Peter Kemoi akitajwa kuwa mnadhimu wa Wengi. Uchaguzi huu ulifuatia kujiuzulu kwa watangulizi wao baada yao kutokubaliana. Kabla yao, kiongozi wa Wengi alikuwa MCA wa Londiani Vincent Korir huku mnadhimu akiwa Haron Rotich.

January 13, 2023