BY ISAYA BURUGU,7TH SEPT,2023-Vyuo vikuu na taasisi zingine za elimu ya juu humu nchini vimetakiwa kushirikiana na tassisi zingine za elimu ya juu baranai Afrika na kwingineko ulimwenguni ili kuimarisha uwezo wake kutoa mafunzo bora Zaidi yatakayowawezesha wasomi kufanikiwa katika ulimwengu wa sasa haswa katika soko la ajira.Wito huo umetolewa na makamu war ais nchini Namibia Nangolo Mbumba.Akizungumza na wandishi Habari hivi leo, jijini Nairobi,Mbumba pia amewataka vijana kukumbatia masomo ya sayansi ili waweze kuzikabili ipasavyo changamoto za kileo .

Mbali na hayo makamu huyo wa rais   wa taifa la Namibia magharibi mwa Kenya amezitaka serikali za mataiafa ya Afrika kujitahidi kuondoa vikwazo vya kimpaka na maeneo ili kuwawezesha raia wa mataifa yao kutangamana hatua ambayo anadai itafanikisha maendeleo na azimio la Afrika moja yenye ustawi.

September 7, 2023