Wakfu wa Safaricom kwa ushirikiano na serikali ya kaunti ya Narok wametia saini mkataba wa matibabu utakaowawezesha wakaazi wa kaunti hii kupokea huduma za afya bila malipo yoyote.

Kulingana na mwenyekiti wa wakfu huo Joseph Ogutu mkataba huo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitatu ijayo huku akiwahimiza kina mama kutafuta huduma za kujifungua hopitalini ili kuzuia madhara wakati wa kujifungua.

Kwa upande wake Gavana wa kaunti hii ya Narok Patrick Ntutu amesema kuwa ofisi yake Iko tayari kuwasaidia wananchi wa Narok kupokea matibabu ya hali juu licha ya tabaka lao.

September 7, 2023