Wabunge wamepata afueni baada ya Mahakama ya Rufaa kubatilisha uamuzi uliotolewa na mahakama kuu mnamo Septemba 20, 2024 kuhusu uhalali wa hazina ya Maendeleo ya Maeneobunge (NG-CDF) kufuatia kesi iliyowasilishwa na Bunge la kitaifa.
Katika hukumu iliyotolewa Ijumaa asubuhi, jopo la majaji watatu linalojumuisha Rais wa Mahakama ya Rufaa Jaji Daniel K. Musinga, Jaji Francis Tuiyott, na Jaji A. O. Muchelule, mahakama ya rufaa iligundua kuwa Mahakama Kuu ilifuta Sheria nzima kimakosa bila kufanya uchambuzi wa kutosha wa maandishi na kanuni za kikatiba, hasa kuhusu masuala ya fedha za umma, ugatuzi, na mgawanyo wa madaraka.
Aidha Wanjiru Gikonyo na Cornelius Oduor Opuot waliiarifu rasmi Mahakama ya Rufaa kuhusu nia yao ya kupinga uamuzi wake uliounga mkono uhalali wa hazina hiyo ya 2015.
Katika notisi ya tarehe 6 Februari, 2026, walalamishi hao walisema kwamba hawakuridhika na hukumu na amri zote za Mahakama ya Rufaa.

