Wahadhiri kutoka chuo kikuu cha Egerton wametoa ilani ya siku saba kwa wakuu wa chuo hicho wakilalamikia kutolipwa mishahara yao.Wakizungumza na waandishi wa habari,wahadhiri hao wameeleza kuwa kwa miezi sita sasa hawajalipwa mishahara na marupurupu yao.Wameongeza kuwa licha ya kufanya mazungumzo kadhaa na wakuu wa chuo hicho bado hawajaweza kuafikiana huku wakieleza kuwa wameshindwa kukidhi mahitaji yao ya kila siku.

October 5, 2022