BY NEWSDESK,25TH JULY,2023-Wakaazi wa eneo la kona katika kaunti ndogo ya Tana delta wanaishi kwa hofu baada ya kupoteza mifugo wa tuhuma za maji ya sumu katika bwawa la kipekee la maji eneo hilo.Wanadai kuwa wamepoteza Zaidi ya ngombe mia tatu katika kipindi cha miezi mitatu baada ya kuyanywa maji hayo.Wakiongozwa na Isa Molu wakaazi hao sasa wanaitaka serikai kuingilia kati na kuwaokoa kutokana na hasara Zaidi.Kijiji cha kone kiko kilomita 180 kutoka mji wa Garasen na kinapakana na mbuga ya Wanyama pori ya tsavo mashariki ambapo kumekuwa na mizozo ya mara kwa mara kuhusu umiliki wa ardhi huku shirika la utunzaji Wanyama pori nchini KWS wakidai kuwa Kijiji hicho kiko ndani ya mbuga hiyo.

.

 

 

 

 

July 25, 2023