BY ISAYA BURUGU 27TH MARCH,2023-Wito umetolewa kwa wakazi wa Trasmara magharibi kuwa wangalifu kufuatia mvua kubwa inayoendelea kushudiwa eneo hilo. Akizungumza eneo la Shangoi Trasmara magharibi Muhamed Nur amesema wakazi wawe macho hasa wanapofunga mto ili kusuia maafa.

Naibu kamishana huyo amesema kuna wale wanahatarisha maisha yao kufuga mito maji ya mafuriko yanapotokea .Nur amesema wengi wameadhrika pakubwa na mvua ya mafuriko kila kunaponyesha maeneo mbali mbali eneo hilo.

Wakati uo huo kamishana huyo ametoa wito kwa wanafunzi wa shule kuwa wangalifu kufuatia mvua kubwa. Nur amesema serikali imetoa tahadhari kwa wasimamizi wa mashule kuhakikisha wanafunzi wote wamefika manyumbani wanapotoka shuleni jioni.

 

 

 

 

 

 

March 27, 2023