BY ISAYA BURUGU 27TH MARCH,2023-Usalama umeimarishwa sehemu mbali mbali  jijini Nairobi siku ambayo  Azimio unandaa mandamano.Polisi walianza kuwekwa katika maeneo mbalimbali mwendo wa usiku wa manane huku maafisa wakati fulani wakiweka vizuizi vya barabarani kukagua magari yanayotumia barabara.SHughuli za uchukuzi pia zimetatizika katika baadhi ya barabara huku  wahudumu wa matatu wakisusia biashara ya uchukuzi.

Mitaa ya katikati mwa jiji (CBD) imesalia bila watu huku wafanyibiashara na wasafiri wakiamua kukambaa  mbali.Kwa kawaida, mitaa ya jiji hujaa watu wanaoendelea na shughuli zao za kila siku mapema kama saa kumi na moja asubuhi.Uchunguzi uliyofanywa na idhaa ya redio Osotua umebaini kuwa maeneo ya Kenya National Archives, Afya Centre na karibu na iliyokuwa hoteli ya Hilton, ambayo kwa kawaida huwa na watu wengi, yamesalia karibu tupu.Polisi wanaonekana wakilinda doria mitaani huku askari hao wakitawanya aina yoyote ya mikusanyiko ikiwa ni pamoja na zaidi ya watu wawili.

Wakati huo huo  maafisa wa polisi wamewarushia vitoa machozi  wandamnaji wa Aziio La umoja  waliokuwa wakiandamana eneo la Mathare.Wandamanaji hao waliwatupia polisi mawe kaika siku ya pili ya mandamano ya kupinga serikali.katika mtaa wa kibra wandamanaji hao wameweka bayana sababu zao za kuandamana.

Usalama umesalia imara wakati maafisa wa polisi wakukabiliana na ghasia wakiwekwa katika sehemu mbali mbali ndani na nje ya Nairobi.Shughuli nyingi za uchukuzi zimesalia kukwama. Kinara wa Azimio Raila Odinga amewashauri wananchi  kundamana kila jumatatu  na Alahamisi kufuatia kile alichokitaja kuwa gharama ya juu ya kimaisha na serikali inayosema si halal

March 27, 2023