Tume ya Kitaifa ya Huduma za Polisi (NPSC) imewatahadharisha Wakenya kupuuza tangazo ghushi la kuwaajiri maafisa wa polisi ambalo limekuwa likisambazwa kwenye mitandao ya kijamii.
Katika taarifa, Tume hiyo iliweka wazi kwamba taarifa zote rasmi kuhusu kuajiriwa kwa polisi zitatolewa tu kupitia njia zake za mawasiliano zilizothibitishwa.
Hizi ni pamoja na tovuti rasmi ya NPSC, vyombo vikuu vya habari na jukwaa la mitandao ya kijamii lililothibitishwa la Tume hiyo. Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mwenyekiti wa NPSC Dk.Amani Yuda Komra, imethibitisha kuwa kwa sasa maandalizi ya zoezi la uajiri halali yanaendelea.
Tume hiyo ilisisitiza dhamira yake ya kutoa masasisho sahihi kupitia majukwaa yaliyoanzishwa na kuonya kwamba taarifa yoyote nje ya njia hizi inapaswa kuchukuliwa kuwa ya uwongo.
Press Statement on Fake Recruitment Advertisement for Police Constables pic.twitter.com/o4AFRAfQqO
— National Police Service Commission – Kenya (@NPSC_KE) September 9, 2025